BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI WA AWAMU YA PILI KWA KOZI ZA AFYA KATIKA MKUPUO WA SEPTEMBA 2022/2023
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi yatatoka tarehe 12 Septemba 2022. Hivyo dirisha la awamu ya tatu litakuwa wazi kuanzia tarehe 12 Septemba, 2022 hadi tarehe 23 Septemba, 2022.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)
08/09/2022